What do you want to learn?

Browse all programmes  
No programmes matching {{ filters.name }}

News

Home | News | Serikali kuendelea kuwekeza kwenye elimu ya juu

Serikali kuendelea kuwekeza kwenye elimu ya juu

Serikali kuendelea kuwekeza kwenye elimu ya juu

SERIKALI KUENDELEA KUWEKEZA KWENYE ELIMU YA JUU

Serikali itaendelea kuwekeza kwenye elimu ya juu katika  Sayansi , Teknolojia na Hesabu,  Hayo yamesemwa Juni 23, 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Hamphrey Polepole alipofanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na  Serikali katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknnolojia Mbeya.

Polepole amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa Maktaba ya Chuo na Hosteli ambazo zitaleta mazingira mazuri ya kujifunzia wanafunzi.

Pia Katibu wa Itikadi na Uenezi ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kwa kusimamia vizuri ujenzi na kutumia fedha za miradi hiyo kama ilivyokusudiwa na kutaka Taasisi nyingine kufuata mfano wa MUST.

Akitoa mada katika Kongamano lililoandaliwa na serikali ya wanafunzi, Pole pole amewaasa vijana waache kulalamika na watambue kwamba  kuongoza nchi ni kazi ngumu kwani kila eneo linahitaji fedha na maeneo yote ni muhimu kwa ustawi wa taifa,  hivyo Serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha kila eneo linapata fedha kwa wakati ili kuleta maendeleo  katika nyanza zote.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Prof.  Aloys Mvuma amemshukuru Rais Magufuli na Serikali kwa ujumla kwa kuweza kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa  Maktaba na Hosteli za Wanafunzi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, amefanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUSTSO) kuwa mzungumzaji mashuhuri katika Kongamano la Fursa za Kilimo na Biashara kuelekea Uchumi wa Viwanda.

 

Imeandaliwa na

Kitengo cha Uhusiano na Habari

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya