What do you want to learn?

Browse all programmes  
No programmes matching {{ filters.name }}

News

Home | News | MUST Yasaini Mkataba wa Kuunda Baraza la Wafanyakazi

MUST Yasaini Mkataba wa Kuunda Baraza la Wafanyakazi

MUST YASAINI MKATABA WA KUUNDA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) imesaini mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi wa Chuo hiko leo tarehe 5/10/2022.

Mkataba huo umesainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Aloys Mvuma, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi stadi, Habari na Utafiti (RAAWU) Bw. Daniel Sinkonde, pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya juu (THTU) Bw. Emmanuel Mwangomo.

Wengine walioshuhudia tukio hilo ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bi. Judith Egina, Afisa Utumishi Bi. Mote Mahenge, Afisa Uhusiano wa Chuo Bw. Dickson Msakazi, Katibu wa RAAWU tawi la MUST Bi.Theopista Mng’ong’o na Katibu wa THTU tawi la MUST Bw. William Innocent.

Mkataba huo ni matokeo ya utekelezaji wa sera ya kuwashirikisha wafanyakazi katika uongozi wa pamoja mahali pa kazi kama ilivyoelekezwa na agizo la Rais no 1 la mwaka 1970 pamoja na sheria ya ajira na mahusiano kazini no 6 ya mwaka 2004 kifungu cha 73 (1-3).

Downloads

Click here to download