What do you want to learn?

Browse all programmes  
No programmes matching {{ filters.name }}

News

Home | News | MUST NA AMSHAAMSHA FOUNDATION WAINGIA MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA

MUST NA AMSHAAMSHA FOUNDATION WAINGIA MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA

MUST NA AMSHAAMSHA FOUNDATION WAINGIA MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA

 Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimeingia makubaliano ya ushirikiano (Memorandum of Understanding - MoU) na Amshaamsha Foundation (AAF) mnamo tarehe 3 Mei 2024, kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo.

Akiongea katika hafla hiyo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Technolojia Mbeya Prof. Aloys Mvuma, aliushukuru uongozi wa Amshaamsha Foundation kwa kuwa tayari kufanya kazi na MUST huku akisisitiza kuwa Chuo kipo tayari kushirikiana katika kutekeleza malengo ya mashirikiano.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Amshaamsha Foundation Bi Theresia Mcha aliushukuru uongozi wa Chuo kwa kukubali kuingia makubaliano na kuahidi kutekeleza yale yote yaliyopo kwenye makubaliano hayo.

Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia Mbeya na Amshaamsha Foundation wamekubaliana kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo maendeleo ya teknolojia ya mionzi, kilimobiashara, na mabadiliko ya tabianchi.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Technolojia Mbeya kimekuwa kikiingia katika makubaliano ya mashirikiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa kwa lengo la kutanua wigo wa huduma zinazotolewa na Chuo ambazo ni kufundisha, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu.