What do you want to learn?

Browse all programmes  
No programmes matching {{ filters.name }}

News

Home | News | KAIMU MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA ATOA RAI KWA WANAFUNZI KUSOMA VITABU

KAIMU MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA ATOA RAI KWA WANAFUNZI KUSOMA VITABU

KAIMU MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA ATOA RAI KWA WANAFUNZI KUSOMA VITABU

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Prof. Aloys Mvuma ametoa rai hiyo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Maonesho ya Huduma za Maktaba (Library Exhibition Week) uliofanyika katika viwanja vya Maktaba ya Dkt. Magufuli.

Akisisitiza umuhimu wa kutumia Maktaba, Prof. Mvuma alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa fedha  nyingi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Chuo ikiwa ni pamoja na kununua vitabu na kompyuta. Aidha, jumla ya vitabu 7,861 vimenunuliwa chini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (Higher Education for Economic Transformation - HEET); juhudi zote hizi zimelenga kuongeza ufanisi wa Maktaba hii kwa watumiaji.

Akiongea mapema wakati wa kumkaribisha Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Godliving Mtui alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kujenga mazoea ya kusoma vitabu vya kiada na ziada pamoja na machapisho mbalimbali yakiwemo magazeti ili kujenga na kuongeza uelewa wa mambo mbalimbali. 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba Bw. Novatus Luanda alisema kuwa waliandaa Maonesho hayo ili kutoa elimu juu ya huduma zinazotolewa katika Maktaba ya Dkt. Magufuli na namna ya kupata huduma hizo, ambapo mpaka sasa huduma zinazotolewa ni pamoja na huduma za vitabu, huduma ya vitabu na machapisho katika mfumo wa kidigitali na wavuti mbalimbali za kitaaluma.

Maonesho ya Wiki ya Maktaba yalifanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 2 Mei mpaka tarehe 4 Mei 2024 kwa lengo la  kutoa elimu juu ya huduma zinazotolewa na Maktaba kwa wanafunzi, walimu na watumiaji wengine wa Maktaba ya Dkt. Magufuli.