Leading Centre of Excellence for Knowledge, Skills, and Applied Education in Science and Technology
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Zanzibar, Mh. Amosi John Henock, ametembelea banda la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) katika Maonesho ya 7 ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja.
Akiwa katika banda la MUST, Mh. Henock alipata fursa ya kujionea bunifu mbalimbali zinazowasilishwa na chuo, zikiwemo teknolojia ya Multitenant Electric Meter inayorahisisha usimamizi wa matumizi ya umeme katika majengo yenye wapangaji wengi, pamoja na teknolojia ya kutengeneza viuatilifu vya asili vinavyotokana na mimea, vinavyosaidia kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao kwa njia rafiki kwa mazingira.