Leading Centre of Excellence for Knowledge, Skills, and Applied Education in Science and Technology
Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Makenya Maboko amefanya ziara ya kikazi katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - Kampasi ya Mtwara (MUST - Mtwara Campus), leo Juni, 2026.
Katika ziara hiyo ya kikazi, Mwenyekiti wa Tume amepokelewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Prof. Said Ali Vuai na kutembelea miundombinu ya kufundishia na kujifunzia iliyopo katika chuo hicho.
Aidha, katika ziara hiyo, Prof. Maboko ameambatana na Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya chuo hicho.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za Tume katika vyuo vikuu vyote nchini ikiwa ni sehemu ya jukumu lake la kufuatilia na kutathmini maendeleo pamoja na changamoto za vyuo vikuu ili kutoa ushauri katika maeneo yanayohitaji uboreshaji.


